Tanzania got it's Independence on 1961 and Kenya got theirs on 1963..
Kenya is already a Second World Country while Tanzania is still on the list of Poorest countries..
Fact_1
Pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tshs. 1,996,000 na Pato la Mkenya kwa mwaka ni Tshs. 3,176,000..
Pato la nchi (Tanzania) ni Tshs. Trillion 98.36 na Pato la nchi kwa Kenya ni Tshs. Trillion 140..
Fact_2
Tanzania kuna madini ya kila aina, Tanzanite, Dhahabu, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Chuma, Kenya hawana madini ya aina yeyote lakini bado wametuzidi pakubwa kwenye pato la Taifa.. Sekta ya madini inachangia 3.3% kwenye pato la taifa kutokana na mikataba mibovu uliyowekwa na viongozi wa CCM.
.
Fact_3
Kenya taratibu inautawala Uchumi wa Tanzania, tayari wana Bank mbili zinazofanya kazi nchini (KCB and Equity Bank), Tanzania bado hatuna Bank yeyote Kenya.
Supermarkets za Kenya tayari zimeingia nchini na kuuwa zetu (Nakumat tayari imeshainunua Shoprite (T), UCHUMI Supermarkets).. Sisi Imalaseko Supermarkets zilishakufa kule Kenya.
Soko la Hisa Dar Es Salaam (DSE) lina Jumla ya Kampuni 21, kati ya hizo Kampuni 7 ni za Kikenya lakini Soko la Hisa la Nairobi (NSE) lina zaidi ya Kampuni 64 na hakuna kampuni hata moja ya Kitanzania.. Hii ni mbaya sana kiuchumi..
Fact_4?
2004 Tanzania tulikuwa na Ndege mbili za serikali (Air Tanzania) na Kenya walikuwa na Ndege 19 (Kenya Airways-KQ)..
2015 Tanzania tuna Ndege 1 ya kukodi kwa ajili ya kupigia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kenya wana Ndege 47 zinazotua katika viwanja 62 vya mabara yote duniani...
Tukumbuke bila kuwa na Shirika letu la Ndege Utalii tunaongelea ni kazi bure..
Fact_5
Wakenya wanacheza smart games na Watanzania bado tumelala..
After Precision Airlines (PA) kuwa threat kwa operation za Kenya Airways (KQ) route za Tanzania na Kenya, KQ wakaingia ubia na PA very smartly na wakawa wanaihujumu undercover. Leo hii PA iko hoi na tayari Operations za Jomo Kenyatta-KIA, Jomo Kenyatta-Mwl. Nyerere zimerudi kwa KQ...
Pili, baada ya TBL kuruhusiwa kuuza bia Kenya, na Kenya walete bia zao Tanzania. TBL wakakaribia kuuwa bia za Wakenya huko kwao wakati huo bia yao TUSKER ikawa haifanyi vizuri hapa Tanzania. Wakavunja makubaliano, ili kila mtu afanye biashara yake kwake. After years EABL ya Kenya ikaingia ubia na SBL na wakaipa License ya kuzalisha na kusambaza TUSKER hapa nchini.. Smartly EABL wanauza hapa kwetu wakati sisi TBL haiuzi kule kwao..
Wakati hayo yote yanafanyika Watanzania tunalazwa na fikra za kijinga za viongozi wetu wa CCM.. Education Matters alot ndio maana UKAWA tukaja na 1.ELIMU 2.ELIMU 3.ELIMU tumeona mbali
Fact_6?
Wakati Kenya wao wakifungua mipaka yao na kwenda kufanya Biashara na uwekezaji na kutafuta ajira kila mahali, Serikali ya CCM imetufundisha uoga na kutojiamini.
Serikali ya CCM inatuambia tukiingia kwenye soko la ajira la Afrika Mashariki Wakenya watatupiga bao. Swali ni kwanini?? Ni kwasababu serikali ya CCM inajua haitoi elimu bora, wanafunzi tunaishia kukaririshwa na walimu wetu wanataka uandike alichokariri yeye kinyume na hapo umefeli na ili akili zetu zisifunguke na kuanza kufikiri sawasawa.. Mfumo mzima wa elimu unatakiwa kuwekwa sawa, na hicho ni kipaumbele cha kwanza cha EL, Kipaumbele kikubwa cha Magufuli ni kugawa Laptops kwa walimu wote nchini.kana kwamba ndio hitaji lao.
Fact_7
Serengeti National Parks ni mbuga bora iliyoshika namba moja kwa Afrika, na Ngorongoro ikiwa namba 5.. Masai Mara ya Kenya ni namba 8. Lakini pia Tanzania tuna Mlima Mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro ambao pia ni kivutio kikubwa cha Utalii..
Lakini maajabu ni kwamba Kenya wanakusanya pato kubwa sana kwenye Utalii kuliko Tanzania. Mwaka 2013 pamoja na matukio ya kigaidi Kenya ilitembelewa na watalii million 1.4 wakati Tanzania yenye amani tele ilitembelewa na watalii million 1.04.. Amani wanayoihubiri CCM na vivutio vyetu vya Utalii bado havijatufaidisha chochote..
Fact_8
Bandari ya Dar ambayo ina feed Tanzania, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia na Malawi ina wastani wa kuingiza Kontena Million 12 kwa mwaka, wakati Bandari ya Mombasa inayofeed Kenya, Uganda na Sudan pekee inaingiza Kontena Million 22 kwa mwaka.
Hivyo bandari ya Mombasa inayolisha nchi 2 pekee (kwa kiasi kikubwa) inaingiza pato kubwa kuliko Bandari ya Dar ambayo inalisha nchi 5.. Tatizo ni nani?? kama siyo CCM..?
?#?Fact_9
Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kilikuwa kinazalisha TYRE bora kabisa za kazi. Kilikuwa na Soko kubwa Afrika Mashariki na kati. Gari zote za Tours zinazotembea porini Afrika Mashariki yote na Afrika ya Kati zilikuwa zinafunga TYRE ya GENERAL. Hata wale wapigana vita za msituni huko Kongo na Sudan walikuwa hawaendi kupambana bila kuhakikisha Land Rover yake imefungwa Tyre ya General. Magari ya serikali yote yalikuwa yanafunga Tyre ya General..
Kiwanda kilikuwa kinalipa kodi isiyopungua Billion 100 kila mwaka.. CCM wakafanya hujuma kukiua, zinatolewa subsidy zinaishia kwenye matumbo yao. Wakenya walivyosmart wakaiba ile Technology ya Tyre za General wakafungua kiwanda chao huko kwao kikaitwa YANA Tyre ambaye sasa ndiye Supplier mkubwa wa Tyre Afrika Mashariki na Kati.. Kampeni zinaanza wamejifanya kuifufua General Tyre, Je, wataweza kupambana na Yana Tyres?? Kenyans are always SMART kuliko akili za CCM
CCM wanasema hapa ni Kazi tu.. hahaha
Fact_10
Yote kwa Yote.. Kenya wametuzidi kila kitu, almost everything..
Mpaka mwaka 2002, Tanzania na Kenya hatukuwa na gap kubwa sana kiuchumi. Kenya wameanza kukimbia kwa Speed baada ya kukiondosha Chama cha KANU madarakani. Watanzania wenzangu, Change is INEVITABLE.. Nchi yetu kwa RASILIMALI tulizonazo tunapaswa kuwa kwenye League na South Africa na Nigeria. Wakenya walipaswa wawe wanazamia hapa TZ kama Wamozambique wanavyozamia kule South Africa.
Mwaka 1992, Uchaguzi Mkuu wa Kwanza wa Vyama vingi ZAMBIA Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zambia alikwenda kwa Rais wa wakati huo wa Zambia KENNETH KAUNDA na kumpa matokeo halisi ya kura zilizopigwa na waZambia na matokeo ya kura zilizochakachuliwa. Mwenyekiti wa Tume akamwambia KAUNDA wanaenda kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa. KAUNDA akawaambia wasubiri, akatoka akaenda bustanini kwake, akapiga magoti akamwomba MUNGU. Kisha akarudi kwa Mwenyekiti wa Tume akamwambia aende akatangaze matokeo yaliyopigwa na Wazambia. TANZANIA tunahitaji busara kama hii iwaingie viongozi wetu, wakubali kutangaza matokeo ya kura zilizopigwa na WATANZANIA.. Viongozi wetu wakumbuke tu, sote tutapita lakini Daima TANZANIA itabakia.
kama ilivyo ahadi yetu hata hapa nimetoa elimu bure
0 Comment to "THIS IS UNFAIR-HUU NDIO UKWELI WA HASIRA YANGU"
Post a Comment