Saturday, September 26, 2015

SIRI NZITO YA TAREHE YA KUZALIWA MTU WA WATU EDWARD LOWASA.

Jina lake ni chimbuko ukoo wa kifalme wa uingereza. Dola ambayo vita kuu ya I ya dunia lilitawala Tanganyika chini ya umoja wa mataifa. wakati Edward lowasa akizaliwa sir Edward Twing-ing alikuwa ana miaka minne tangu aje Tanzania kama Gavana. Jina la Edward lina maana ya WEALTHY GUARDIAN kwa kimombo kwa tafsiri ya kiswahili cha huku machakani Basi huyu ni Mlezi au Kiongozi aliyejaliwa utajiri wa watu...

TAREHE YAKE YA KUZALIWA YABEBA SIRI NZITO.

Tarehe ya kuzaliwa mhe. Edward lowasa yabeba ujumbe mzito.
Wadadisi wa Maandiko ya Kikristo Wanatuambia kuwa namba zina maana pana zaidi ya kuonyesha idadi ya vitu au kiasi. Waingereza wanasema ``Numbers are beyond numerical value''
Ili tuweze kuelewa dhana hii hebu tuchukulie mfano wa namba SABA. Katika biblia namba hii inamaanisha UKAMILIFU (fullness)
Twende taratibu katika injili ya Mathayo 18:22. Petro anamuuliza Yesu ndugu akinikosea nimsamehe mara saba (7)? Yesu akamjibu Sikwambii mara saba bali hata mara sabini (70). kimsingi hakuwa anamaanisha asamehe mara 490, bali asamehe kikamilifu tena mara zote. Kwa jinsi hiyo sasa tukubaliane kwa kibiblia namba ni zaidi ya idadi ndugu!!
Mhe. Edward lowasa aliteuliwa kugombea urais tiketi ya ukawa kupitia chama cha chadema.
Mhe. Edward Lowasa alizaliwa tarehe 26/08/53. Unaweza kuona kwa ujumla wa Tarakimu za Siku, Mwezi, Mwaka ni Nane (8).
Haya Twende: Tarehe ya kuzaliwa 26 ambayo (2+6=8), Mwezi wa 08 ambao(0+8=8), Mwaka 53 ambao(5+3=8). Isitoshe mwezi nane (8) mwaka huu Edward lowasa katimiza miaka 62. (6+2=8)pia ukichukua mwezi huu wa nane na miaka anayotimiza ukijumlisha unapata ni yale yale Nane (8).
MAANA YA NAMBA NANE (8) KIBIBLIA NI÷
Katika biblia nane inamaanisha Mwanzo mpya. Mifano ni Mingi Tunasoma katika Biblia kuwa Mungu aliumba Mbingu na Nchi kwa Siku Sita ya Saba akapumzika, Kwahyo Siku ya Nane ni MWANZO MPYA!!!!
Yesu alifufuka Siku ya kwanza ya juma. Tunajua kuwa juma lina siku Saba(7), Basi siku ya Kwanza ya juma ni siku ya Nane (8).MWANZO MPYA .

Watoto wa kiume walitahiriwa siku ya Nane(8). Katika agano jipya, Tohara ya moyoni ni kumpokea Roho mtakatifu na kuwa kiumbe kipya, kuzaliwa mara ya pili yaani MWANZO MPYA!! (Rum 2:28-29, kol 2:11-13, 2k or 5:17).
Yesu alisema maneno Saba (7) Msalabani neno la saba likiwa ''Imekwisha'' Akakata roho. Kwahiyo neno la Nane ( 8 ) Alilisema baada ya kufufuka yaani, Alipoanza MWANZO MPYA!!.
Je, Umesahau kuwa Mungu Aliokoa watu Nane (8) Katika Safina ya Nuhu ili Aanze MWANZO MPYA wa dunia ya Watu Baada ya Gharika?
Je, Mwaka 2015 ni Mwaka gani wa Watanzania? (2+0+1+5=8) Ni Mwaka wa Mwanzo Mpya?
Je, Mwaka 2015 ni MWANZO MPYA wa Mhe.Edward lowasa Kuongoza Tanzania Mpya, yenye Chama kipya, na Mabadiliko Mapya.

Tukiondoka kwenye maandiko ya kikristo, Pia watalamu wa elimu ya namba (numerology) nao hawajatuacha. Wanatuambia kuwa namba 8 ina nguvu kubwa zaidi kwani inawakilisha mamlaka,Biashara, Pesa, na fani (Authority, Business, Finance and Career).(www.numerology.com/numberology-number/8).

Ngoja mtaalam michael kombe a.k.a Mayor Nikupe Zawadi nyingine maana umesoma sana ujumbe wangu kwa muda mwingi sana.

Mwalimu Julius Nyerere Alizaliwa Tarehe 13/04/22 Sasa angalia Jumla ya hizi Namba.
Mwl. julius Nyerere alizaliwa 13/04/22 Haya Twende. Tarehe ya kuzaliwa 13 (1+3=4), Mwezi 04 (0+4=4), Mwaka 22 (2+2=4).

Je, Unajua maana ya Nambari nne (4)? Nambari nne huwakilisha kutotetereka vilevile huonyesha msingi madhubuti (Stability and Strong Foundation). Je dhana hizi zinahusiana vipi na sifa aliyokuwa nayo baba wa Taifa?
Kuhusu Nelson Mandela, Tarehe yake ya kuzaliwa na sifa alizokuwa nazo ndo utajua tarehe hiyo ya kuzaliwa viongozi hawa zina siri nzito mno!!! Mtaalam naacha kama ``Home Work".

Politicts whatsapp 0767679627

Share this

0 Comment to " "

Post a Comment