MBINU ZA KUMUUA MBATIA ZAFICHULIWA,NCCR WADAI WAMEPATA MKANDA MZIMA,WASEMA YA DK MVUNGI YANAMYEMELEA MBATIA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini NCCR Mohamed Tibanyendera akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam |
CHAMA cha NCCR mageuzi kimepata taarifa mbaya juu ya watu wanaotaka kumvamia na kumua Mwenyekiti wa chama hicho Taifa James Mbatia kutokana na harakati zake za ukombozi za kukiondoa chama cha Mapinduzi CCM madarakani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akifichua mbinu hizo chafu Mwenyekiti wa baraza la wadhamini Mwanasheria mkuu wa chama hicho Mohamed Tibanyendera leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa ambapo amesema Idara ya usalama ya chama hicho imepata taarifa ambazo anasema ni za kuaminika za kwamba kuna makundi ya kitaalamu ambayo yameandaliwa kwa ajili ya kumvamia Mbatia na kumdhuru.
Amesema mbali na mbatia makundi hayo pia yamepanga kuwadhuru viongozi wengine wa NCCR ili kuweza kuwafanyia unyama huo.
Tibanyendera amesema taarifa hizo zimetanabaisha kuwa watu hao wamepangwa kufanya vurugu mbalimbali katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi kwa kuwavamia na kuwafanyia ghasia viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA huku wakiwa wamevalia sare za chama hicho
Hata hivyo Tibanyendera amesema kwa mujibu wa taarifa hizo mlengwa mkuu wa katika mpango ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia, jambo ambalo amesema hawataweza kukubali kwakuwa yatakapo tokea yatakuwa na athari kubwa katika chama hicho.
Vilevile Tibanyendera amesema hatua za awali alizochukua mwenyekiti wao ni kutoa taarifa makao ya Jeshi la Polisi nchi juu ya matishio hayo.
0 Comment to "MBINU ZA KUMUUA MBATIA ZAFICHULIWA,NCCR WADAI WAMEPATA MKANDA MZIMA,WASEMA YA DK MVUNGI YANAMYEMELEA MBATIA,SOMA HAPO KUJUA "
Post a Comment