Na C.P Lekule
HUENDA NI KWA SABABU YA LOWASSA KUWAKIMBIA
Pamoja na sera za wapinzani kua na soko,na hili nalo huenda ni moja wapo,
Ni ndoto ambayo nitaiandika baada ya kufikisha ujumbe huu,
Ila pia kuna jambo hapa ninalowaza kabla eti ni kweli yote haya ni sababu ya wanasiasa nguli watatu waliohamia UKAWA ndio wanaofanya serekali inatapatapa na kuongea mambo yaliyopo nje ya katiba kama ni kweli navyohisi CCM wanajikaanga kwa mafuta yao,kwani hawana pa kukwepea,wapinzani sasa ni akili kubwa iliyowaelemea,wakitoa mwanya tu raisi atadumu miaka miwili.
Lakini jiulize maswali haya
Je raisi ni mkuu wa Sumatra yote Tanzania?
Je raisi ni mkuu wa kila wizara Tanzania?
Je katiba wapi inaeleza kua raisi ndie mkuu wa kila kitu? Na kama ipo hiyo sehemu na wake zetu wote ni wakwake tunasubiri tamko tu, si kama miaka ile ya wafalme,mke mzuri wa.......ngombe nzuri ya .....na vingine vingi hebu
Twende kwenye andiko kwa sababu nikiifikiria nchi yangu nachoka namuomba Mungu kila kukicha aipooze hasira yangu juu ya nchi na viongozi wanaoniudhi,tutauliwa,kwa siri na damu itabaki ikiisaidia nchi, siketi hata siku moja nikimuombea kiongozi asiejielewa sawa.!
Naiandikia polisi leo,nikiwa mwenye butwaa kubwa sana,imenibidi niandikie polisi wa aina zote swala hili najua kabisa kua polisi ni baba zetu,polisi ni mama zetu,polisi ni dada na kaka zetu,wengine ni wajukuu na watoto wetu, awali ya yote namshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kuandika tena huu ujumbe,pia niwashukuru wote wanaonielewa niandikapo jumbe mbalimbali kwa kushauri jambo fulani au kulikosoa nikiwa naelewa kushauri au kukosoa sio uchochezi kama inavyotafsiriwa sasa,mimi ni mwanachama hai mpinzani napaswa kukemea na kushauri serejali kwa nguvu zote, hii ni saa 8 usiku nimeashtuka usingizini na kusikia nafsi ikiniambia niandike hili swala,machozi yameujaa moyo wangu,na ni kweli kwamba heri ujisikiapo kulia lia mpaka uchungu uishe kabisa kwani machozi ni sumu sanyingine,ndio maana hata msibani mtu anapolia mwache huwezi jua kakumbuka lipi,mtoto anapoanguka akakuta unamwangalia hulia zaidi ila akikuta haujamwona hunyamaza peke yake,kuna satu pia ukiwabembeleza waliapo huongeza kilio ndio maana nasema anaelia mwache akiisha maliza kulia,mfuate na umshauri au uzungumze nae mambo yatakayomtoa kwenye kilio hicho,baada ya mimi kulia sana nimemaliza nikanawa uso wangu,na kuanza kuandika,wazo kubwa ikiwa ni kuhusu kauli ya KUTII SHERIA BILA SHURUTI inaumiza sana unapomlazimisha raia ambaye ni ndugu yako akubali kutopigania haki yake ya kikatiba,kwasababu ya amri ya mkubwa fulani,mimi ningekua askari ningesimamia katiba na kama huyo anaeniagiza yuko nje ya sheria naanza nae,tukubaliane hakuna alieko juu ya sheria,na kama ndio hivyo kwanini polisi mnapelekwa kwenye mkumbo wa kushiriki kuivunja katiba, hebu fikirieni tunaohitahi haki yetu kikatiba ni ndugu zenu,haki ikipatikana sio kwa ajili yetu peke yetu na kwa ajili pia ya ndugu zenu,je kwanini mnapelekeshwa kana kwamba hamna elimu? Au ndio tuanze kujifikiria kua polisi wote ni wale waliofeli? Mbona nawafahamu polisi wengi wenye elimu,mbona hamtoi kauli,kumbukeni hawa mnaotumwa kuwakandamiza ilihali wako sahihi kikatiba wakiingia serekalini,mishahara yenu haipungui,au ndio tuseme mmemisi vita,kazi yenu hasa ni nini? Kama sio kutulinda tudaipo haki zetu,? Polisi tusijenge uadui na raia kwani nchi nyingi zilipoteza amani kwa mambo kama hayo,watu walishindwa kuvumilia kuminywa kwa haki zao na wakajitoa kwa ajili ya wengine inaumiza sana,
Kuna point mbaya sana inajengwa na baadhi ya viongozi,raisi anasimama na kuhubiri ukanda na ukabila anapigiwa makofi ndie alietakiwa ahukumiwe haraka kwa ubaguzi anaofanya,jambo ambalo ni hatari sana,viongozi wengi wanashindwa kujua wao kua kwenye nafasi fulani sio kwamba wao ni bora sana au wana akili kuliko wengine la hasha wapo wenye akili zaidi yao ila wana nafasi nyingine,mengi yanayofanywa na serekali iliyopo madarakani ni kinyongo kwa sababu ya Lowassa yaani kumkomoa eti kwanini kahama,hiyo ni haki yake,kwa wanaoifuatilia siasa naamini hata Lowassa angehama CCM kipindi cha Mh.Kikwete wapinzani wangeandamwa sana,hii inadhihirisha ni mtu mwenye nguvu polisi nao wanaingizwa kwenye mission bila kujua,zamani enzi za wafalme mfalme alikua akisikia mtu anasifiwa zaidi yake yuko radhi auwawe sifa zote ziletwe kwake,ndio yanayotokea sasa,ila naamini kizazi hichi ni cha tofauti sana wengi wao wamefunguka sio waoga tena, wanapigana sio tu kwa ajili yao na pamoja na kizazi kijacho,TUPIGANE KWA AJILI YA KIZAZI KIJACHO.
0 Comment to "HUENDA NI KWA SABABU YA LOWASSA KUWAKIMBIA"
Post a Comment