Tuesday, August 30, 2016

Dikteta

::Madikteta wote duniani hufanana::

Kutoka Maktaba (JF by Mzee Mwanakijiji 
11 Feb 2011 ) #UKUTA

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!

Monday, August 29, 2016

JIFUNZE KUMUACHA AENDE

JIFUNZE KUMUACHA AENDE

• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!

Tupo pamoja??

Share na marafiki zako wajifunze

Hadithi ya kusisimua

KAMA UNA MOYO MWEPESI USISOME STORY HII,
WENGI WAMELIA SANA !!
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu
aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na
kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu
alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari
kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha
anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza
kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili
ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu.
Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake
aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali
lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na
akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule,
hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa
kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini
kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika
nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha;
alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia
kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote
yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa,
niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke
wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa
30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana
vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana
mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa
muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza
kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu
kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti
mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia.
Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.
Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa
majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa
jambo la hakika zaidi.
Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana
nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani.
Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda
moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara
moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula
raha za kufa mtu na Mary
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado
akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na
kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya
talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu
lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa
kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika
kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye
tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa
kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo
lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia
kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo
hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya
kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali
mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada,
aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate
yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi
kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe
nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa
kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa.
Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro
nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.
Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na
mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata
akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’,
alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu
hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya
kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza
sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga
makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama
mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni
moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni,
halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi
nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema
kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu
ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia
vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami
nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili,
zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani
pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye
blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa
makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua
hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na
nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula
urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini
namfanyia hivi.
Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu
zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na
tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita
ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea
upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri
mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke
wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya
kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.
Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua
mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna,
‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua
kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo
maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo
likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu
makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa
kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema
‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’.
Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo
la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara
mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo
mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo
katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi
mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka
mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka
shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake;
ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi
wake ulinitia mashaka.
Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga
hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni.
Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba
maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini….
Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana
nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua....
nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia,
‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.
Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa
changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake
kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki
kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na
furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu,
mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani.
Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu
nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu,
nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo
kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao
cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia.
Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye
duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili
ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye
kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila
asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”.
Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu,
tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani,
nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.
Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani
kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu
nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba
angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na
mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume
mwema.
Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.
Kama Stori Hii Imekugusa Na Ungependa Marafiki Nao
Waisome Basi Unaweza kusambaza

Sunday, August 28, 2016

KATIBA-Haki ya uhuru na mawazo

Na C.P Lekule KATIBA 3-Hebu angalieni katiba inavyokanyagwa kanyagwa hapa kuna ibara zinalihusu BUNGE LIVE jamani watanzania tusiwe wajinga woa wakitumia mipasho kutuhukumu sisi tutumie sheria.
HAKI YA UHURU NA MAWAZO
Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.
Uhuru wa mtu
kuamini dini
atakayo Sheria
ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria ya 1992
Na.4 ib…
19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
20
Uhuru wa mtu
kushirikiana na
wengine Sheria
ya 1984 Na.14
ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au
kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au
mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake
za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya
Muungano;
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na
kwa njia za kidemokrasia.
(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti
yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na
vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu
uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.
(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa
kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
Uhuru wa
kushiriki
shughuli
za umma
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67
ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya
kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki
katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa
nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi
waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia
utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
_________________________________________________________________
21
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu
katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha
yake au yanayolihusu Taifa.

KATIBA-Haki na wajibu muhimu

Na C.P Lekule KATIBA 1-HAYA NI MAELEZO KATIKA KATIBA YA JAMUHURI YA TANZANIA-gundua jambo hapa kwamba polisi wanaotoa matamko ya ajabu ajabu ni kinyume cha katiba hii kama wanatumia katiba nyingine sawa ila kama ni hii matamko yote ni haramu,yana ubaguzi,yanaondoa usawa,yanatuvunjia heshima,katiba hii haijasema kua polisi au waziri au DC au OCD au IGP kua ana haki zaidi na ana uwezo wa kuivunja au kuikanyaga katiba hebu soma kidogo,pia nawashauri wanasheria wa UKAWA hawa wanaojifanya wao kambale kauli zisizo wahusu wanazitoa pelekeni mahakamani watueleze katiba inayowaruhusu kufanya hivyo.
SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa
Usawa wa
binadamu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
12.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake.
Usawa mbele
ya Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa
mujibu wa sheria.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
17
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii
neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji
mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,
kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,
jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina
fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa
aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida
iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno
"kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali
kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha
matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya
kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,
heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote
zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu
anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama
au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
____

KATIBA-ijue Haki ya kuishi

Na C.P Lekule KATIBA 2-Mtanzania hebu ijue haki yako ya kuishi kikatiba,hao bongo lala wanaosema ukija Dar es salaam usikae sana,wanalala wakiamka asubuhi bila hata kufikiri wanatoa matamko ya kipuuzi yanayokinzana na katiba katiba yetu inasema hivi;-
HAKI YA KUISHI
Haki ya kuwa hai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
14. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii
hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.
Haki ya Uhuru
wa mtu binafsi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
15.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama
mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na
kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini,
kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake
vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu
iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na
mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Haki ya faragha
na usalama wa
mtu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi
kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na
unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na
mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa
ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu
hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya
usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza
kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
Uhuru wa mtu
kwenda atakako
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya
kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri
ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye
madhumuni ya-
_________________________________________________________________
19
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na
kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu
kwenda anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu
wowote anaotakiwa na sheria nyingine
kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au
kuhifadhi maslahi fulani mahususi au
maslahi ya sehemu fulani ya umma,
kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo
haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara
hii.

Friday, August 12, 2016

HUENDA NI KWA SABABU YA LOWASSA KUWAKIMBIA

Na C.P Lekule
HUENDA NI KWA SABABU YA LOWASSA KUWAKIMBIA
Pamoja na sera za wapinzani kua na soko,na hili nalo huenda ni moja wapo,
Ni ndoto ambayo nitaiandika baada ya kufikisha ujumbe huu,
Ila pia kuna jambo hapa ninalowaza kabla eti ni kweli yote haya ni sababu ya wanasiasa nguli watatu waliohamia UKAWA ndio wanaofanya serekali inatapatapa na kuongea mambo yaliyopo nje ya katiba kama ni kweli navyohisi CCM wanajikaanga kwa mafuta yao,kwani hawana pa kukwepea,wapinzani sasa ni akili kubwa iliyowaelemea,wakitoa mwanya tu raisi atadumu miaka miwili.
Lakini jiulize maswali haya
Je raisi ni mkuu wa Sumatra yote Tanzania?
Je raisi ni mkuu wa kila wizara Tanzania?
Je katiba wapi inaeleza kua raisi ndie mkuu wa kila kitu? Na kama ipo hiyo sehemu na wake zetu wote ni wakwake tunasubiri tamko tu, si kama miaka ile ya wafalme,mke mzuri wa.......ngombe nzuri ya .....na vingine vingi hebu
Twende kwenye andiko kwa sababu nikiifikiria nchi yangu nachoka namuomba Mungu kila kukicha aipooze hasira yangu juu ya nchi na viongozi wanaoniudhi,tutauliwa,kwa siri na damu itabaki ikiisaidia nchi, siketi hata siku moja nikimuombea kiongozi asiejielewa sawa.!

Naiandikia polisi leo,nikiwa mwenye butwaa kubwa sana,imenibidi niandikie polisi wa aina zote swala hili najua kabisa kua polisi ni baba zetu,polisi ni mama zetu,polisi ni dada na kaka zetu,wengine ni wajukuu na watoto wetu, awali ya yote namshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kuandika tena huu ujumbe,pia niwashukuru wote wanaonielewa niandikapo jumbe mbalimbali kwa kushauri jambo fulani au kulikosoa nikiwa naelewa kushauri au kukosoa sio uchochezi kama inavyotafsiriwa sasa,mimi ni mwanachama hai mpinzani napaswa kukemea na kushauri serejali kwa nguvu zote, hii ni saa 8 usiku nimeashtuka usingizini na kusikia nafsi ikiniambia niandike hili swala,machozi yameujaa moyo wangu,na ni kweli kwamba heri ujisikiapo kulia lia mpaka uchungu uishe kabisa kwani machozi ni sumu sanyingine,ndio maana hata msibani mtu anapolia mwache huwezi jua kakumbuka lipi,mtoto anapoanguka akakuta unamwangalia hulia zaidi ila akikuta haujamwona hunyamaza peke yake,kuna satu pia ukiwabembeleza waliapo huongeza kilio ndio maana nasema anaelia mwache akiisha maliza kulia,mfuate na umshauri au uzungumze nae mambo yatakayomtoa kwenye kilio hicho,baada ya mimi kulia sana nimemaliza nikanawa uso wangu,na kuanza kuandika,wazo kubwa ikiwa ni kuhusu kauli ya KUTII SHERIA BILA SHURUTI inaumiza sana unapomlazimisha raia ambaye ni ndugu yako akubali kutopigania haki yake ya kikatiba,kwasababu ya amri ya mkubwa fulani,mimi ningekua askari ningesimamia katiba na kama huyo anaeniagiza yuko nje ya sheria naanza nae,tukubaliane hakuna alieko juu ya sheria,na kama ndio hivyo kwanini polisi mnapelekwa kwenye mkumbo wa kushiriki kuivunja katiba, hebu fikirieni tunaohitahi haki yetu kikatiba ni ndugu zenu,haki ikipatikana sio kwa ajili yetu peke yetu na kwa ajili pia ya ndugu zenu,je kwanini mnapelekeshwa kana kwamba hamna elimu? Au ndio tuanze kujifikiria kua polisi wote ni wale waliofeli? Mbona nawafahamu polisi wengi wenye elimu,mbona hamtoi kauli,kumbukeni hawa mnaotumwa kuwakandamiza ilihali wako sahihi kikatiba wakiingia serekalini,mishahara yenu haipungui,au ndio tuseme mmemisi vita,kazi yenu hasa ni nini? Kama sio kutulinda tudaipo haki zetu,? Polisi tusijenge  uadui na raia kwani nchi nyingi zilipoteza amani kwa mambo kama hayo,watu walishindwa kuvumilia kuminywa kwa haki zao na wakajitoa kwa ajili ya wengine inaumiza sana,

Kuna point mbaya sana inajengwa na baadhi ya viongozi,raisi anasimama na kuhubiri ukanda na ukabila anapigiwa makofi ndie alietakiwa ahukumiwe haraka kwa ubaguzi anaofanya,jambo ambalo ni hatari sana,viongozi wengi wanashindwa kujua wao kua kwenye nafasi fulani sio kwamba wao ni bora sana au wana akili kuliko wengine la hasha wapo wenye akili zaidi yao ila wana nafasi nyingine,mengi yanayofanywa na serekali iliyopo madarakani ni kinyongo kwa sababu ya Lowassa yaani kumkomoa eti kwanini kahama,hiyo ni haki yake,kwa wanaoifuatilia siasa naamini hata Lowassa angehama CCM kipindi cha Mh.Kikwete wapinzani wangeandamwa sana,hii inadhihirisha ni mtu mwenye nguvu polisi nao wanaingizwa kwenye mission bila kujua,zamani enzi za wafalme mfalme alikua akisikia mtu anasifiwa zaidi yake yuko radhi auwawe sifa zote ziletwe kwake,ndio yanayotokea sasa,ila naamini kizazi hichi ni cha tofauti sana wengi wao wamefunguka sio waoga tena, wanapigana sio tu kwa ajili yao na pamoja na kizazi kijacho,TUPIGANE KWA AJILI YA KIZAZI KIJACHO.

Tuesday, August 2, 2016

JE NIFUNGUE KESI MAHAKAMA GANI KWA HAWA WANAONICHOCHEA KUA MUHALIFU?

JE NIFUNGUE KESI MAHAKAMA GANI KWA HAWA WANAONICHOCHEA KUA MUHALIFU?

Na C.P Lekule
Huyu mtu hanikwazi peke yangu kwa kauli zake,je ule mfano wa msichana akibakwa kama mavazi yalikua yanachochea yeye kubakwa naye anapewa adhabu hapa je haiwezi kutumika hiyo sheria,mimi kiukweli kuna baadhi ya viongozi wa nchi wananishawishi kuwa gaidi,yaani nakua na msukumo hadi wa kujiunga na vikundi viovu, je nikawashtaki wapi hawa wanaopekekea mimi kuwaza maovu? Je hakuna wakunishauri kesi yangu niipeleke wapi,na kuna mmoja wao nasikia hatakiwi kushtakiwa basi bashauri ambaye hashtakiwi na akifanya jambo yeye ni sahihi,basi hata yeye asiwe na haki ya kushtaki;_ naomba nizungumze ninachokijua mpaka sasa viongozi baadhi wa ngazi za juu ccm, wanajifunza namna ya kuijua hasira yangu,mimi ni mtanzania nina sumu ya amani mda mrefu,mkiigeuza kua vita ni kali zaidi ya sumu ya nyoka, namkumbuka wajina langu kabla hajafariki aliniambia,kuvunjika kwa mlango viti na meza uhofia,pia pia akaniambia paka halii nyau mpaka asikie harufu ya samaki au amuone samaki,bado naelezea ukurasa huu una maana kwa wenye akili ya grade A
Leo katika kurasa yangu ninaongezea kufafanua maana ya neno siasa,hapo zamani tulifunzwa na tukaelezwa pamoja na vitabu vingi kua maana ya neno siasa ni.
"... mawazo, mipango na busara za kuendesha nchi au jambo lolote". Kutokana na tafsiri hiyo basi ni dhahiri kua kila sekta tanzania inahitaji siasa ,kilichonifanya niandike hii nimeona watu wengi,wakifata mkumbo na kulitafsiri neno siasa vibaya,kuna madokta,walimu,maaskari,watu wenye elimu ya juu wamekua wakikosa adabu ya kutafsiri neno hili na kuliharibu siku hadi siku, ukizungumza jambo kwa maelezo mazuri sana utaambiwa unafaa kua mwanasiasa hiyo ni kweli,na pia ukiwa mpigania ukweli utasikia watu wanasema yule mwanasiasa ni kweli,ila sasa unapomkosoa mtu kwa kutumia haki utaambiwa usinichanganye na siasa zako,utasikia watu wanasema taaluma sio siasa tena watu wenye akili,huwa nasikitishwa sana watu wameshindwa kujua taaluma yoyote ni siasa,siasa iko kila mahali,siasa ndio maisha ya kila siku.Ndio maana mwalimu Nyerere akasema "siasa ni kilimo" sasa nashangazwa na raisi wa awamu hii kua dikteta hadi kwenye kiswahili,eti anasema siasa zinakwamisha maendeleo,bila kujua hata yeye yuko kwa ajili ya siasa,nimelazimishwa na watu kurudia kurasa hii,kwani tanzania inapoteza dira kwa kila jambo,raisi amekua msemaji wa kila wizara,na kutumia polisi kuwahujumu na kuwatisha wapinzani,wasiikosoe nchi hatutoacha kusema,kwani raisi alitakiwa kuiongoza nchi,na sio kuitawala kama anavyofanya sasa, mimi napenda kumuheshimu kiongozi yoyote anaeongoza kwa haki sio kidikteta, demokrasia ipo ila haitumiki vizuri,mimi ni kati ya watu wanaochukia kauli ya wengi wape,kwani tanzania tumekua tukiwapa wapumbavu wengi mamlaka ya kutuendesha kijinga na bado tunatulia tu.
Na kusema chaguo la Mungu tunamdhihaki Mungu kila kukicha,sio Tanzania tu afrika imekua ya ajabu sana, kwa sababu kila mtu amekua akimtegemea mwenzie aseme jambo,hata kama jambo linamuumiza atashukuru tu,ila mimi sikulelewa kusema nyeupe ni nyeusi,napenda kusema nyeupe ni nyeupe na nyeusi inabaki kua nyeusi tu, polisi wa Tanzania fanyeni kilicho haki sio kupelekeshwa na mtu fulani,itafika mahali tutaheshimiana tu, nitasimamia ukweli tu mara zote,na sitaacha mpaka nchi iwe kwenye mwelekeo wa haki,

Wananchi Hawajaribiwi

Naomba Mh.Raisi Maghufuli kama haupendi kujaribiwa na Wananchi pia hawapendi kujaribiwa,tena ukiendelea kuwajaribu hawa wananchi wakibadilika utajutia kua Raisi wa Tanzania,na wala hufuati nyayo za mwalimu Nyerere na wala huwezi,mambo mengi unakurupuka,nchi haiendeshwi kwa matamko hata siku moja,acha kuajiri watu kwa kukurupuka,nasema hivyo kwa sababu umekua ukiajiri watu masaa machache umewatengua,maana yake umekurupuka,unawanyima haki wapinzani,kwa sababu unawaogopa kiutawala,yaani unatakiwa uelewe kua raisi sio kwamba una akili zaidi ya wananchi wote,elewa kuna wenye akili zaidi yako, hivyo usituongoze kama umetawala Matahira tafadhali,siku machafuko yakitokea kwa kusababishwa na utawala hohehahe utawajibishwa kimataifa kinga haitasaidia,unaemkandamiza,unayemnyanyasa,unayemnyima haki siku akijua hakutakalika nchi itakua ndogo sana hii japo ni kubwa,mtu asiependa kukosolewa ana udhaifu wake mkubwa,hajui kuongoza anakua anahofia ubaya kuzidi wema wake,hakuna mwenye haki miliki ya nchi hii,tunakuomba kama ulichaguliwa halali, ongoza si utawale enzi za ufalme zilishaisha,acha kuweka historia mbovu katika nchi yetu,tunaumia kwa sababu nchi hii sio yetu peke yetu kuna vizazi na vizazi vijavyo, sio kila anaekosoa serekali apewe kesi ya uchochezi, Mwalimu Nyerere na wenzake wawili enzi za chama kimoja waliwahi kushtakiwa kwa kosa la uchochezi baadae kukaja vyama vingi sheria ilitakiwa kurekebishwa ila bado,HATARI YAJA TUSIPOKUA VIONGOZI MAKINI.