Saturday, July 2, 2016

KILIMANJARO by CV


KUTOKA KWA CP Lekule
KWENDA KWA ;_Waziri wa utalii
               Mh.Jumanne Magembe

YAH;KAZI ZA MSIMU HASA GUIDE NA POTER MLIMA KILIMANJARO.
Barua kwako waziri wa utalii JUMANNE MAGEMBE
Uandishi wa bazua za wazi untumika sana zama hizi Mh.enzi zile ilikua ngumu kwa sababu ya utandawazi kutokuwepo,tulikua tunatumia majani,karatasi,mawe na hata magome ya miti kufikisha ujumbe fulani mahali,ila siku hizi mambo mepesi kabisa,ni jambo la heri sana pia kwetu kufikisha mambo kadha wa kadha,kwa viongozi mbali mbali,natumaini yoyote atafikisha ujumbe huu kama hautakua online leo au kesho,kichwa cha habari hapo juu chahusika,
UTANGULIZI;_kama unavyoelewa kazi hizi zilivyo ngumu,muheshimiwa,ila kwa ufafanuzi mdogo tu,utafahamu
Nilianza utalii 2003 nikiwa kama mpagazi nilikua nikienda shule na baadae natoroka kuelekea kwenye kazi hiyo kupata matumizi madogo madogo na ada

Tulipambana kiukweli ila kila penye mkusanyiko walaji hawakosekani kazi hii ya kubeba mizigo ya watalii kwenda mlima kilimanjaro ni ngumu sana kiasi kwamba heri hata jeshini yaani namaanisha ukiwakusanya waliozoea ile kazi ukawapeleka jeshini wataona wako mapumzikoni, kipindi hicho kila kampuni zilikua na malipo tofauti ila mimi nilikua napanda na kampuni iliyokua inalipa elfu kumi na tano 15000 kiukweli ilikua hela kubwa sana na nilikua nina uwezo wa kufanya
kazi chache tu nikalipa ada na kumaliza matumizi mengine,ila baada ya mda lilianzishwa shirika lililodai ni la kutetea wapagazi na kua linachukua au linamega kiasi cha mshahara wa wapagazi eti kwamba ukifa watakusaidia au ukiugua,tulipambana na waanzilishi wa lile shirika kwani ulikua ni utapeli
Kwani sikuona kua linamsaada wowote lilikua ni kupe kwa wapagazi.

Kwa sababu kazi ile ni ya msimu na ndio maana kuna low season na high season,hivyo fedha zetu walizokua wanachukua hazikua na faida kwetu wakanitishia watanifunga,sikuchoka kuhoji naviongozi ambao pia nawafahamu kwa majina wa Kilimanjaro Nation Park walikua ndio wanawapa nguvu hawa matapeli kwa kujua au kutokujua mara ghafla baada ya shirika hilo kujikusanyia fedha za kutosha likapotea ghafla minongono mingi sana ilibaki japo wapagazi walisahau kutapeliwa kule na kuendelea na  kazi zao za msimu mara baada ya mda liliibuka tena likijiita Kilimanjaro Poter Asociation bado wakapewa nguvu kubwa zaidi na viongozi baadhi wa Kilimanjaro Nation Park pamoja na baadhi ya matour operators baadhi kwa maslai yao binafsi,na wengine mkumbo ili waitwe viongozi,kwa hili lazima kuna faida waliyokua wanaipata kwenye hilo shirika ninaloliita halikua likitenda haki lakini bado sikukaa kimya nilihoji na nikaonekana mkorofi, kama ilivyo tanzania ukiongea ukweli unachukiwa mkorofi.Sasa kwa mpagazi kukipata kitambulisho yaani kukipata kitambulisho ilikua 15000 bila kitambulisho huingii msituni,hubebi mzigo(chamanda,gas,mburuta na nk) ndio kauli ya yaani kitambulisho kinachoitwa cha  KPA ndio kinachohitajika sio cha kura wala mkazi, badala wapambane namna ya hawa wapagazi kupata stahiki zao wanahangaika kupunguza stahiki za wapagazi kwa kushirikiana na viongozi baadhi wa KINAPA,

Mashirika yako zaidi ya moja ada yao ni zaidi ya elfu 40 kwa miezi sita bado wanahitaji ujiunge na bima na uikorokoro kibao, hapa najiuliza kujiunga na shirika lolote duniani kikatiba ni hiyari je mbona huku ni lazima na kwanini KINAPA CHINI YA TANAPA MNAHALALISHA HUU UNYONYAJI KWA KAZI ZA MSIMU? kwa nini nasema kinapa chini tanapa wanashiriki hawa ndio sapoti ya hawa wanaotengeneza mashirika ya kinyonyaji, mimi najiuliza kuna maana gani ya kuweka mafunzo ya  uongozaji wageni na kutoa leseni ilihali ukija na mgeni leseni haina maana tena unaulizwa kitambulisho cha shirika lingine,kwanini kila tour operator au kampuni yenye tin number zisifanye haya mambo peke yao kwa sababu kila kampuni ina usajili wa wao.goza wageni na wapagazi wake na hata waongoza wageni kipindi cha mafunzo ya kitalii matour operator au kampuni ndio hutoa majina na yakapitishwa na KINAPA na sio shirika KGA au hayo mengine, kiukweli mimi mnanichanganya bado pamoja na barua hii nitakuja kwenye ofisi zenu tuzungumze tena ili nifahau nisichokijua na nyinyi pia mfahamu msichokijua

Share this

0 Comment to "KILIMANJARO by CV"

Post a Comment