Saturday, July 2, 2016

Funzo Kwa kizazi cha Utawala

Na CP Lekule
Tatizo kubwa nimeliona,wenye macho ambao kwa bahati nzuri ni wengi zaidi ya vipofu, nao nadhani wameliona,wapo walioliona wakashindwa kulisema japo wanatamani kusema,wengine wanakuja chinichini nakutuombia tuseme sisi tuliojaliwa kutokua na dhambi ya woga kwa mtu bali kwa Mungu tu,mtu unaposhindwa kua na watendaji wazuri,huenda hata sehemu uliyopo  ni bonge la suprise kwako so unashangaa kuapale ulipo kwani hukupatarajia hivyo unashangaa shangaa huku siku za utendaji zikiyoyoma,kwani ni sawa na mtu ambaye alikua hawazi kabisa kua hata boyfriend wa mtu leo hii anashangaa yuko kanisani au msikitini anafungishwa ndoa,pia kuna kiongozi hajawahi kuota hata siku moja kua mwenyekiti wa kitongoji, leo hii anashangaa kutajwa kiongozi wa ngazi ya juu, mfano mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa,mbunge,waziri,spika,naibu spika, na nk. Sasa ubaya wa uongozi unaoupata kua surprise ni kujikuta unapoteza weledi wa uongozi,na ndipo unapotofautiana na wenzako kwa kujiona wewe ndio wewe,wewe ndio final say wa kila kitu,kila jambo linahitaji maandalizi,viongozi wengi wazuri waliandaliwa,sasa mfano viongozi wa kwenye madhehebu mbalimbali na nk, Mwalimu nyerere hakukurupuka tu na kujikuta baba wa taifa,Amani Karume pia vivyo hivyo, achana na hao wa hapa wakina Kwame Nkuruma,Adolf Hitler,Saadam Husen,Gadafi na wengine kibao waliandaliwa hawakufanyiwa surprise kama viongozi wengi wa ccm walivyofanyiwa surprise,tuje kwenye maandalizi ya uongozi,kiongozi unaweza andaliwa na matatizo yanayoibuliwa ndani ya nchi,na viongozi wa namna hii huwa na vision kubwa ya kumlinda kila mtu,kiukweli kiongozi wa maandalizi ya namna hii huwa mzuri zaidi ya maandalizi yote,viongozi wa namna hii mara nyingi hupenda haki na mara nyingi nchi nyingi hushindwa kuhujumu nchi iliyotawaliwa na viongozi wa namna hii,hatimaye yanapotokea machafuko yoyote viongozi wa namna hii huweza kushinda kwa maana ya kwamba uzuri wao ndio huanza kujulikana zaidi na hata wapotezapo maisha hawafutiki katika historia.

Kuna viongozi ambao huandaliwa kindugu au kichama kwa kuandaliwa kwa namna hii,hakudumu sana katika uongozi,kiongozi wa namna hii mara nyingi hujikuta wanatawala kifalme badala ya kuongoza na nchi nyingi huingia kwenye machafuko au vita na mara nyingi hawaishindi vita,viongozi wa namna hii wengi hupinduliwa kijeshi,huwa hawakubali kung'ooka,viongozi wa namna hii huwa na vision ndogo tu hasa huwa na malengo na ndugu au chama na huwa na dharau mara nyingi,pia hua wanajitoa sana kuwalinda waliowaweka kwenye huo uongozi,hujaribu kulazimisha kua wao ndio wanaweza zaidi,kuliko wengine,huwafanya matajiri wakubwa wanaoshika uchumi kua upande wao,na wakionekana wako kinyume,huuwawa au kufungwa gerezani kwa mda mrefu sana,ili kuwapotezea vision,hutaka kuabudiwa japo maranyingi hufanya kinyume cha sheria, je tunaona nini tukiangalia kesho bila haraka,na tukiangalia kesho kwa haraka haraka,machozi tumeshayaona,jasho pia damu,je tunayoyafanya ni kwa ajili yetu peke yetu? Mzalendo hupigana kwa ajili ya kizazi kijacho,yu heri ateseke ila mwanae au mjukuu wake aishi kwenye amani,je kuna mtu anapigana kwa ajili ya watoto wake au ndugu waje kuishi vitani? Mzalendo hukubali kuishi vitani ila baadae wanaofuatia waishi kwa amani, mimi nitasimamia ukweli japo ukweli unawaumiza wanafiki wengi,viongozi wanaowajengea wananchi nidhamu ya woga,sio viongozi,pia kiongozi anayependa kukosolewa ndie kiongozi mzuri,ila anayeogopa kukosolewa huyo kashapima kua hana uwezo wa kukaa alipo,MUNGU ibariki Tanzania.

Share this

0 Comment to "Funzo Kwa kizazi cha Utawala"

Post a Comment