Rais John Pombe Magufuli
AKIHUTUBIA kwenye uzinduzi wa darala la Kigamboni jijini Dar es Salaam mchana huu, Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na kuisababishia serikali hasara ya pesa zaidi ya bilioni 3.
Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo ripoti ya tume aliyounda kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009 ambapo ule wa mwaka 2004 ulipelekwa jiji na ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa basi linatozwa sh. 4000 kwa siku wakati mzabuni anatozwa 8000 kwa sikuKutokana na maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na ameagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa
0 Comment to "KABWE KWELI KWELI"
Post a Comment